Habari

Kauli 10 za M/kiti wa CCM, Rais Magufuli akizungumza na Viongozi wa CCM Dar (+Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka kuzungumza mafanikio ya serikali yake kwenye mkutano na viongozi wa CCM na Jumuiya zake ikiwa ni miaka 5 toka aingie madarakani mwaka 2015.

Hizi ni kauli 10 ambaye amezitoa Rais Magufuli kwenye mkutano huo ambao amefunguka kuzungumzia mambo mbalimbali.

Hizi ni kauli 10 ambazo amezitoa Rais Magufuli kwenye mkutano huo ambapo amefunguka kuzungumzia mambo mbalimbali.

1. “Nani alitegemea nchi iwe na Ndege, mwezi unaokuja tunaanza safari za Ndege kutoka hapa hadi China moja kwa moja, Ndege nyingine zinakuja na tumenunua Cash, tajiri huwezi nunua kwa kukopa.” Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Viongozi wa CCM.

2″Huwezi ukapewa Nchi tajiri kama hii halafu maendeleo yakwame, siku za nyuma kila siku Dar msongamano, tumeona kama nikujenga flyover tutandike kila mahali flyover. Tuliweka tsh Bil 600 ndio maana kila mtaa Dar barabara za lami” Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli

3. “Huwezi ukapewa Nchi tajiri kama hii halafu maendeleo yakwame, siku za nyuma kila siku Dar msongamano, tumeona kama nikujenga flyover tutandike kila mahali flyover. Tuliweka tsh Bil 600 ndio maana kila mtaa Dar barabara za lami” Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli

4. “Jambo jingine ninalolisisitiza ni ushirikiano baina ya Chama na Serikali. Lengo letu sote ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu, na hakuna ubishi kuwa CCM ndio chama kinachotawala hivyo hakuna sababu ya kutofautiana na kulumbana” Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli

5. “Hatutaki Chama hiki kuwa ombaomba ambacho kinategemea matajiri ambao baadae wamekuwa wakikiweka Chama mfukoni.” Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Viongozi wa CCM.

6.”Fedha zilizopo sasa hivi tuna uwezo wa kuendesha nchi kwa miezi 6, hatakama tusipokusanya leo hela tunaweza kuendesha nchi kwa miezi 6 ndiyo maana tunapata fedha za kujenga miradi mikubwa.” Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli akiwa na Viongozi wa CCM.

7. “Eneo la fedha na uchumi tumeweza kuchukua hatua mbalimbali kuhakiki, kurejesha na kuthaminisha upya mali na rasilimali za Chama, na jitihada hizo zimeongeza mapato kutoka Tsh Bil 46.1 hadi mwaka 2015/16 hadi tsh Bil 59.8 mwaka 2018/19″Mwenyekiti CCM, Rais Magufuli

8. “Nawashukuru sana wajumbe, kwa kweli leo nina raha sana, na kama ndugu Bashiru unafikiri lolote baya leo hakuna baya shetani ameshindwa. Leo ni siku ya raha ya kukutana na Chama kikubwa kilichoshika hatamu ya uongozi wa Taifa hili,” Rais Magufuli na Viongozi wa CCM

9.”Nataka kuwahakikishia wananchi wenzangu kuwa tumeamua, tunaitengeneza nchi. Tunajenga Iringa, Arusha, Manyara, Mwanza, Mara, Dar es salaam na kila mahali mpaka Kagera. Kila mahali maendeleo yameonekana. Sifa hizi sio zangu bali ni zenu nyie wanaCCM Mimi ni mtumishi wenu tu” Mwenyekiti CCM, Rais Magufuli

10. “Leo naenda kushuhudia mkataba wa Barrick wa madini unaenda kutiwa saini na kwamba Serikali itakuwa share na kampuni mpya imeunda inaitwa Twiga mambo ya kudhulumiwa hapana, kiujumla chama kipo safi na Serikali ipo safi” Mwenyekiti  wa CCM, Rais Magufuli

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents