Michezo

Kauli aliyoitoa Wanyama kuhusu Kenya kupangwa na Tanzania AFCON2019″Itakuwa mechi ya watani wa jadi”

Nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya Victor Wanyama amesema kuwa mechi dhidi ya majirani zao Tanzania katika michuano ya AFCON itakuwa ni ngumu sana. Mataifa hayo jirani ya Afrika Mashariki yamo kwenye Kundi C pamoja na mataifa ya Senegal na Algeria.

Harambee Stars ya Kenya itaminyana na Taifa Stars ya Tanzania Juni 27 jijini Cairo na huo utakuwa mchezo wa pili kwa timu hizo.

“Ni kazi ngumu, nilifikiri hawa watu wanataka watu wa Africa Mashariki wapigane,” kiungo huyo wa Tottenham ameiambia BBC huku akitabasamu.

“Najua itakuwa mechi ya watani wa jadi, wao (Tanzania) ni ndugu zetu na itakuwa mechi ngumu pia lakini tupo tayari kwa changamoto hiyo.

“Hakuna hata timu moja ya kuidharau sababu mpaka ufuzu AFCON, inakupasa uwe na timu imara, hivyo tumo kwenye Kundi gumu. Tutajaribu kadri ya uwezo wetu kusonga mbele.”

Taifa Stars
Image captionTanzania imefuzu Afcon baada ya kusubiri kwa miaka 39.

Kenya haikuweza kufua dafu katika michuano ya mwisho waliyoshiriki mwaka 2004 na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Tanzania wao wanashiriki kwa mara ya pili michuano hiyo, mara ya kwanza ilikuwa 1980.

Wanyama pia amesema Harambee Stars hawajajiwekea malengo yeyote kwenye michuano hiyo.

“Hatuna malengo mahususi, itatupasa kucheza kwa bidii mchezo mmoja baada ya mwengine na kuandikisha alama,” Wanyama ameiambia BBC.

“Ni jambo jema kwangu, ni mafanikio ya juu kabisa kuiongoza nchi yangu kwenye AFCON mwaka huu. Tunataka kwenda na kufurahi na kucheza mchezo wa kiwango kilicho bora.”

Mchezo wa kwanza wa Kundi C utawakutanisha Tanzania na Senegal Juni 23. Kenya wataanza michuano hiyo dhidi ya Algeria Juni 23.

Tanzania itamaliza hatua ya makundi dhidi ya Algeria Juni 1, na siku hiyo hiyo na muda huo huo Kenya watakuwa wanaumana na Senegal.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents