DStv Inogilee!

Kauli ya Alikiba kuhusu Diamond kupitisha video za wasanii wa Bongo kuchezwa MTV Base

Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa kituo cha runinga cha kimataifa, MTV Base huwa wanampigia kuidhinisha video yoyote inayotumwa kwenye kituo hicho kutoka Tanzania ili azitolee maoni kama zipitishwe ama laa, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wakiwemo wasanii wenyewe.

kingkiba

Miongoni mwa wasanii waliozungumza kuhusu kauli hiyo ni pamoja na Alikiba, ambaye itakumbukwa kuwa video zake hazioneshwi na kituo hicho, kitu kinacholeta sintofahamu pia kutokana na tofauti zake na Diamond.

“Nitawaambia ukweli ambao unawahusu, kama ni kweli watakuwa wanakosea (MTV), haikai sawa na sidhani kama ni kweli,” alisema Alikiba kupitia 255 ya XXL alipoulizwa maoni yake kuhusu swala hilo.

“Yaani haikai sawa na sidhani kama ni kweli, kwasababu watakuwa hawako fair, ndio hivyo hawako fair, hajabeba talent ya kila mtu (Diamond), kila mtu ana kipaji chake na kila mtu ana haki ya kuonesha kipaji chake kazi yake. Unajua kila mtu anafanya biashara ya muziki saizi, sio mtu anafanya masihara unapoona mtu anafanya video yake anagharamikia unajua haipendezi, kwahiyo sidhani kama ni kweli.” Alisema Alikiba.

Kauli ya Diamond aliitoa alipokuwa akieleza jinsi wasanii wanavyomtupia lawama kuwa anawanyima connections za kung’ara kimataifa, “mimi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mimi najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndio huwa nasababisha” alisema Diamond.

“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwasababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yeyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? Tuicheze ngoma yake au? Mimi huwa nasema anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu.” Alisema Diamond.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW