Kauli ya kamanda Mambosasa baada ya jambazi sugu ‘Kambale’ kuuawa na polisi – Video

Kauli ya kamanda Mambosasa baada ya jambazi sugu 'Kambale' kuuawa na polisi - Video

Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamefanikiwa kumuua jambazi maarufu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Kambale, usiku wa kuamkia Novemba 6, 2019, eneo la Ukonga Mazizini, jijini humo na kumkuta na silaha moja aina ya Bastola.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam

Taarifa hiyo imetolewa Novemba 6, 2019, na Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ambaye amesema kuwa, jambazi huyo alikuwa ni maarufu sana kutokana na matukio yake ya utekaji wa bodaboda na kuwaua watu.

“Katika juhudi zetu za kupambana na uhalifu, tumeua jambazi maarufu sana alikuwa anaitwa kambale, ametesa sana kule Ukonga – Mazizini na Kinyerezi, amekuwa anateka watu na kuwaua bodaboda na kufanya chochote anachotaka na jina la Kambale lilikuwa na maana ya kila akitaka kukamatwa anateleza”, amesema SACP Mambosasa.

Akizungumzia hali ya usalama ndani ya Jiji hilo, Mambosasa amesema kuwa bado wanaendelea kuwasaka wale wote, wanaotaka kuleta taswira tofauti ili kabla hawajatimiza lengo lao wawafikie na Jiji liendelee kuwa salama.

Chanzo Eatv.tv

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW