Burudani

Kauli ya kwanza ya Lady Jaydee baada ya kusaini label ya Taurus Musik

Baada ya msanii wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jadee kusaini kufanya kazi na label yaΒ Taurus Musik amefunguka mambo machache.

Lady Jaydee amesema label hiyo itakuwa ya pili kufanya nayo kazi tangu mwaka 2001, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Lady Jaydee ameandika;

Mara ya kwanza kabisa ku sign na record label ilikuwa 2001 ambapo nili sign mkataba wa Albums 2. Album yangu ya kwanza Machozi 😭😭na album ya pili Binti πŸ’ͺ🏽πŸ’ͺ🏽 Baada ya hapo sikuwahi ku sign tena mkataba mwingine wowote hapo katikati, Bali nilikuwa nafanya kazi na ndugu jamaa na marafiki wa karibu ambao nawashukuru sana kwa mchango wao mkubwa katika kuniendeleza na kunipa moyo.πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½βœŒπŸ½βœŒπŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½βœŒπŸ½βœŒπŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½

Ninapoufunga mwaka 2017 naufunga kwa Neema ya kipekee kwani kwa mara ya pili katika career yangu ya muziki nime sign naΒ @taurusmusikΒ na natarajia mambo makubwa zaidi ya hapo nyuma kwani kila hatua naamini inatakiwa kukusogeza katika kupanda juu zaidi.

Mapenzi tele kwa fans, family, kila mmoja ambae amechangia mimi kuwepo hapa bila kutaja jina la mmoja mmoja, na hata wale tuliotofautiana lakini bado walichangia kufanikiwa kwangu hata kama ni 1% ( huo ni ubinaadam )na watu wote wenye imani na Lady JayDee βœŒπŸ½β€οΈπŸ’‹.

Ila Mama yangu mzazi ndio mwanamke pekee anaenipa nguvu na sababu ya kuendelea mbele kila kukicha ❀️Nani Kama Mama ?❀️#TunasongaMbeleHaturudiNyuma
#SikuYaKuchokaNdioSikuYaKufa
#KeepTheFireBurningπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

Jaydee amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Taurus Musik ya Nigeria ambayo inafanya kazi zake nchini Kenya. Moja ya vipengele vya mkataba huo vilivyoorodheshwa ni kuwa msanii huyo atatakiwa kuachia albamu mbili katika kipindi cha miaka hiyo mitatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents