Tupo Nawe

Kauli ya Manara ya This is Simba yahamia Italia , Kocha wa Juventus asema ‘This is Ronaldo baada ya kufunga

Juventus wamefanikiwa kupata sare ya 1-1 wakiwa ugenini dhidi ya Ajax, jijini Amsterdam, Uholanzi. Ronaldo amepachika goli hilo katika dakika 45′ kwa kichwa safi, na kufikisha magoli 125 akiendelea kuchanja mbuga kama mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwenye historia ya michuano hiyo.

Ronaldo amefunga magoli hayo akiwa na timu tatu, awali Manchester United halafu Real Madrid na sasa Juventus.Mchezaji huyo nguli amenyanyua kombe hilo mara tano. Ajax walisawazisha dakika moja tu baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia David Neres kwa shuti la yadi 15.

Timu zote mbili zilipata nafasi za wazi ambazo walishindwa kuzitumia. Jurgen Ekkelenkamp wa Ajax alipata nafasi ya wazi ambayo iliokolewa kabla ya nafasi ya Douglas Costa wa Juventus kugongesha mwamba.Sasa timu hizo zitaenda kumalizana mjini Turin, Italia juma lijalo.

Baada ya mchezo Kocha wa Juventus alipoulizwa kuhusu mechi kwa Ronaldo baada ya mechi, kocha mkuu Allegri aliwaambia waandishi wa habari: “Alikuwa anawaonyesha kuwa amerudi tu, alikimbia sana na alicheza mchezo mzuri.

“Alianza hatua hiyo na akafunga goli” This is Ronaldo.

“Lakini ningeongeza kuwa katika mchezo wa pili tunapaswa kufanya vizuri kama timu na zaidi ya yote tunapokuwa na goli la ugenini ni vizuri zaidi.”

Mbali na matokeo hayo kwa Juventus hizi ndio takwimu anazoongoza Ronaldo:-

Wafungaji Bora wa Klabu Bingwa Ulaya
JinaMagoliTimu
1. Cristiano Ronaldo125Manchester United, Real Madrid, Juventus
2. Lionel Messi108Barcelona
3. Raul71Real Madrid, Schalke
4. Karim Benzema60Lyon, Real Madrid
5. Ruud Van Nistelrooy56PSV Eindhoven, Manchester United, Real Madrid
6. Robert Lewandowski53Borussia Dortmund, Bayern Munich
7. Thierry Henry50Monaco, Arsenal, Barcelona
8. Andriy Shevchenko48AC Milan, Chelsea, Dynamo Kiev
8. Zlatan Ibrahimovic48Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, Paris St-Germain
10. Filippo Inzaghi46Juventus, AC Milan

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW