Michezo

Kauli ya Mesut Ozil yapelekea CCTV kuifutilia mbali mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City

Shirika la habari nchini China CCTV,  limefutilia mbali kuonyesha mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City inayotarajiwa kupigwa hii leo siku ya Jumapili saa 1:30 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki kufuatia ujumbe uliandikwa na mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil kupitia mitandao yake ya kijamii.

Arsenal's Mesut Ozil criticised China's policies toward its Muslim Uighur minority on Saturday

Ozil alichapisha aliposti ujumbe kwenye akaunti zake za kijamii ambao unakosoa namna Waislamu wa Uighurs wanavyoteswa nchini China.

Kupitia ujumbe huo, Mesut Ozil aliwaita Waislamu hao wa Uighurs kama mashujaa ambao wanapinga unyanyasaji na mateso na kuikosoa China pamoja na idadi kubwa ya Waislamu waliolifumbia macho jambo hilo.

”(Ndani ya China) Qurans zilichomwa, Miskiti ilifungwa, Shule za Kiislamu, Madrasa zilizuiliwa, Wasomi wa dini wamekuwa wakiuawa mmoja kwa mmoja. Pamoja na hayo yote Waislamu wamekaa kimya,” Ameandika Ozil ambaye ni Muislamu kupitia Twitter.

Chama cha soka nchini China kimeiyambia chombo cha habari cha Serikali kuwa kimesikitishwa na sana na matamshi yaliyotolewa na Ozil hawaungi mkono.

”Kauli ya Ozil, imewaumiza sana mashabiki wa China wanaomfuatilia, lakini wakati huo huo ujumbe wake umeumiza hisia za watu wa China. Hiki kitu hatuwezi kukikubali.” Ujumbe kutoka katika chama hicho cha soka.

Gazeti la Global Times limesema kuwa sasa CCTV-5 imeufutilia mbali kurusha matangazo ya mechi hiyo na badala yake itaonyesha mchezo wa Tottenham dhidi ya Wolves.

Hata hivyo Arsenal imesema kuwa ayihusiki na matamshi ya Kiungo huyo raia wa raia Ujerumani ikidai kuwa huwa haijihusishi na mwaswala ya kisiasa na kuongeza kuwa hayo yalikuwa maoni binafsi ya Mesut Ozil.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents