Habari

Kauli ya Rais Magufuli; ‘asihamishwe mtumishi bila kulipwa’, yatolewa ufafanuzi Bungeni

Serikali kupitia Naibu Waziri wa TAMISEMI,Joseph Kakunda imesema kuwa walimu wote waliohahamishwa na wenye madeni halali watalipwa stahiki zao na wale ambao bado wasubiri watahamishwa baada fedha kupatikana.


Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Suzan Lyimo akiuliza swali leo Bungeni jijini Dodoma kuhusu walimu

Kauli hiyo imetolewa na Kakunda leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Suzan Lyimo aliyeuliza “Hakuna kada inayonyanyasika hapa nchini kama walimu, hivi karibuni serikali ilipunguza baadhi ya walimu wa sekondari kwenda shule ya msingi kutokana na upungufu wa walimu na ikadai ina fedha za kuwalipa ,leo tunavyozungumza baadhi ya wakurugenzi wamwaambia wale walimu warudi katika shule za sekondari kwahiyo ina maana serikali ilikuwa haijajipanga, Je ni lini serikali sasa itawalipa walimu hao fedha kama ambavyo mlidai mtawalipa?


Naibu Waziri wa TAMISEMI,Joseph Kakunda akijibu swali la Mbunge Suzan Lyimo

“Kwanza uamuzi ule wa kuhamisha walimu waliozidi katika shule za sekondari wa sanaa wapelekwe katika shule za msingi ulikuwa ni uamuzi sahihi kilichosisitizwa ni kwamba mtumishi yeyote anastahili apate haki zake kama ilivyohainishwa kwenye kanuni zetu za utumishi, Mfano Tangazo la Mh. Rais limetoka mwezi wa pili asihamishwe mtumishi mpaka alipwe wale ambao walishahamishwa na madeni yao halali watalipwa wala hakuna tatizo lakini wale ambao walikuwa bado watasubiri watahamishwa baada fedha kupatikana na wale ambao wamerudishwa wamerudishwa kuwa muda tu naomba hili liwe cleared halina tatizo lolote.

Hata hivyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa asihamishwe mtumishi yeyote mpaka alipwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents