Kauli ya Rapper wa kike Cardi B ya kutaka kujiingiza kwenye siasa ilivyopokelewa na mashabiki zake

Kauli ya Rapper wa kike Cardi B ya kutaka kujiingiza kwenye siasa ilivyopokelewa na mashabiki zake

Rapper wa kike kutoka nchini Marekani, Belcalis Almanzar maarufu kwa jina la Cardi B, aliweka wazi nia ya kutaka kuingia kwenye masuala ya siasa siku tatu zilizopita.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 27, alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuweka wazi nia hiyo kwa ajili ya kutaka kupigania amani kwa wananchi.

“Nadhani natakiwa kuwa mwanasiasa, naipenda serikali japokuwa mambo wanayoyafanya kwa sasa sikubaliani nayo, nimekuwa nikifuatilia video za matukio yanayoendelea ya kivita, bila ya kujali tuna uwezo wa silaha za kivita, watu wanatakiwa kuwa na amani,” alisema Card B.

Msanii huyo aliyetamba na wimbo wa ‘Bodak Yellow’ aliongeza kwa kusema anatakiwa kwenda shule kwa ajili ya kujiweka sawa mambo ya kisiasa ili aweze kuja kuwa mmoja kati ya viongozi bora.

Kutokana na ujumbe huyo baadhi ya mashabiki walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa msanii huyo anafaa kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa 2020 huku wengine wakimtaka agombee 2032.

Mbali na hao waliomtaka agombee miaka hiyo lakini wengine hawakutaka kabisa na walikuwa wakimkatisha tamaa kwa kumwambia wewe gombe ila kura yangu hutaipata kabisa.

Lakini kuna wengine walimshauri aachane na mambo ya siasa bali aendelee kufanya anachofanya sasa hivi akimaanisha usanii.

Mbali na hao lakini pia kuna wengine ambao walienda mbali zaidi wakimwambia kuwa “Inamana hao waliopo kwenye siasa hawawezi bali wewe una mawazo au una uwezo mkubwa kuliko waliopo madarakani?

Lakini pia kuna wengine walimpongeza na kusema CARDI B ndio rais mtarajiwa wa Marekani

Hayo ni baadhi ya maoni ya mashabiki wa rapper huo anayefanya vizuri kwa sasa nchini Marekani na duniani kote lakini pia siku za hivi karibuni alitangaza kuwa anataka kuhamia nchini Nigeria kutokana na machafuzi yanayoendelea kati ya taifa lake la Marekani na taifa la Iran kwamba kuna mzozo wa kivita hivi alitangaza anataka kuchukua uraia wa Nigeria na Serikali ya Nigeria ilimkaribisha kwa mikono miwili na kusema kwamba kama kuna wengine pia wanataka kuhamia au kuchukua uraia wa Nigeria wanakaribishwa.

Je Unahisi Cardi B anauweza Urais au aliongea kutokana na hali inayoendelea kati ya Marekani na Irani ?

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW