Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Kauli ya Safaree kwa ex wake Nicki Minaj yashangaza wengi

Rapper Safaree ameteka vichwa vya habari kutokana na ujumbe wake aliomtumia ex wake Nicki Minaj.

Safaree kupitia mtandao wa Twitter, amewashtua watu kwa kumuandikia ujumbe mpenzi wake huyo wa zamani [Nicki] kuwa anahitaji sana mtoto kutoka kwake.

“I really want a kid. Nicki you were suppose to have my child.. I can’t believe this is life,” ameandika rapper huyo kupitia mtandao huo. Ujumbe huo wa Safaree umekuja muda mchache baada ya mrembo Minaj kupost kipande cha video ya wimbo mpya alioshirikishwa na Future ‘You Da Baddest’.

Ukweli unaonyesha kuwa Safaree bado anamzimia sana Nicki japo mrembo huyo mara kibao ameonyesha kuwa hataki tena mazoea. Wawili hao walidumu kwenye mahusiano kwa takriban miaka 12 kabla ya kumwagana na Nicki kuingia mikononi mwa Meek Mill.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW