Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Kauli ya Waziri Ummy baada ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumuacha katika wizara yake baada ya Baraza la Mawaziri kufanyiwa mabadiliko.

Waziri Ummy ametumia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa wataendelea kupambana na wataacha alama.

Namshukuru Mh Rais @MagufuliJP kwa kuendelea kuniamini kuongoza Wizara hii. Tunapiga hatua, Tunaendelea kupambana na Tutaacha Alama! ??????

Katika hatua nyingine Waziri Ummy alimpongeza Naibu Waziri wake alieteuliwa Dr Faustine huku akimkaribisha katika wizara yake na kuahidi kumpa ushirikiano wa karibu.

Rais Magufuli Oktoba 7 mwaka huu alifanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW