Habari

Kazi ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali yawekwa wazi

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji, ameeleza kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haijawahi kumhusisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukaguzi wa Balozi au ukaguzi wowote ule kama Umoja wa Mataifa.

Hayo yamezungumzwa, Bungeni mjini Dodoma na Naibu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kiwengwa Khamisi Mtwana Ally (CCM), lililohoji;

Ni mara ngapi Ofisi hiyo ya Bara imeishirikisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Zanzibar.

Dkt Kijaju alisema kuwa “Ofisi hizo kila moja ina mipaka yake ya kufanya ukaguzi na kwamba jukumu la ukaguzi wa Taasisi za Muungano lipo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba majukumu ya Ofisi hiyo yameainishwa katika ibara ya 143(2) ya katiba hiyo”. alisema Dkt. Kijaji

“Eneo hilo linamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi angalau mara moja kila mwaka na kutoa taarifa kuhusu ukaguzi wa Hesabu za Serikali, Bunge na Mahakama. Majukumu hayo yameainishwa katika kifungu cha 10 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 na kanuni zake za mwaka 2009.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents