Burudani

Keisha naye kuwania ubunge mwaka huu? Jibu liko hapa

Mzuka wa siasa unazidi kuwaingia wasanii wengi wa muziki nchini. Keisha ni mmoja wao.

11356494_1619032284977479_1841000979_n

Akizungumza na Bongo5, Keisha amesema naye pia ana mpango wa kuingia rasmi kwenye kuwania nafasi ya uongozi wa kisiasa japo inaweza isiwe mwaka huu.

“Napenda sana harakati za siasa, nimeshawahi kufikiria lakini bado sikupata jibu sahihi,” amesema. “Kwahiyo sasa hivi siwezi kusema nipo tayari ama vipi. Lakini nikiwa tayari nitaweka wazi kila kitu. Mimi ni mwana-CCM damu kabisa nimekunywa maji ya bendera.”

Miongoni mwa wasanii watakaogombea ubunge mwaka huu ni pamoja na Profesa Jay na Afande Selle.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents