Habari

Keki hii yazua gumzo, kampuni iliyotengeneza yakiri makosa

Shirika la ndege la Uganda limeadhimisha mwaka wake wa kwanza kwa kukata keki ambayo umbo lake limezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Air Uganda

Air UgandaKampuni iliyooka keki hiyo ilibezwa mitandaoni wikendi iliyopita. Kampuni hiyo imekiri kuwa haikutoa vyema muundo wa ndege ya shirika la ndege la Uganda na kuanzisha shindano la kuoka keki tena hiyo.

Keki

‘’Tulijaribu kutengeza keki ya muundo wa ndege lakini kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii hatukufanikiwa’’

Wito sasa umetolewa kwa waokaji keki wakubwa kwa wadogo kushiriki katika shindano hilo ambalo mshindi atafadhiliwa na kutengeza keki na kupewa nafasi ya kuiwasilisha binafsi kwa shirika la ndege la Uganda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents