Kelis na Nas Waachana

Kelis na Nas Waachana
Habari zilizokuwa zikielezwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu
harakati za kutengana kwa wanandoa Nas na Kelis takribani kwa mwezi
mzima uliopita leo zimethibishwa na msemaji wa Kelis

"Nina thibisha kuwa Kelis ameshasign hati za kuachana na Nas" alieleza wakili Laura Wasser ambaye pia amewahi kuwa wakili wa Britney Spears, Angelina Jolie na Steve Wonder.

Wakili huyu alijaza hati hizo kwa niaba ya Kelis akieleza kuwa ni kwa sababu zisizorekebishika wasanii hao wameamua kila mmoja kula hamsini zake.

Hata hivyo Kelis kwa sasa anaujauzito wa takribani miezi 7 akitarajia mtoto wakiume.
Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa nyota hao wamesikitika huku wakibaki kusema huenda Nas hana bahati na warembo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents