Habari

Kelly Rowland wa Marekani apata dili ya kuwa balozi mpya wa JAGUAR

Guess what, mwimbaji ambaye ni kati ya nguzo tatu zinazoisimamisha brand ya Destiny’s Child, Kelly Rowland amelamba dili ya kuwa balozi wa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari aina ya ‘JAGUAR’ hivyo sio mbaya tukimpa a.k.a mpya ya ‘Jaguar Chick’ (Ila sio wa Kigeugeu)!

kelly-4

Kelly ambaye jina lake kamili ni Kelendria Trene Rowland baada ya kupata deal hiyo ambayo kwa hakika itakuwa ni nono, ameonekana maeneo ya Miami, Marekani katika utengenezaji wa tangazo la kampuni hiyo yenye makao makuu Uingereza.

kelly-2

Kizuri share na wenzako, so Kelly Rowland hakuona ubaya japo kushare na mashabiki wake habari hii njema katika career yake kwa kutweet picha akiwa katika ‘Jaguar F5 model sports car’ zilizosindikizwa na caption hii “Cruisin in my #F-type @jaguarUSA! Shooting commercial latemiaminights The jag is everything! Supersexy!!!”

Kelly-3

Rowland ambaye ni mwimbaji, mwandishi na muigizaji, kwa sasa anai promote album yake mpya na ya nne ‘Talk A Good Game’ ambayo ilitoka (June 14) mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents