Burudani

Kendrick Lamar amzawadia dada yake gari la kifahari

Kendrick Lamar ameamua kuonyesha upendo kwa dada yake katika sherehe ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya sekondari.

Rapper huyo ameamua kumzawadia dada yake huyo anayefahamika kama Kayla Duckworth, gari mpya aina ya Toyota Camry.


Picha ya ndani ya gari ambalo Kendrick amempa zawadi dada yake

Kayla ameonyesha kufurahishwa na zawadi hiyo kutoka kwa kaka yake, kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha inayoonyesha sehemu ya ndani ya gari hilo na kuandika, “Thank you big brother for my graduation gift! ❤️ @kendricklamar.”


Picha ya Kayla akiwa na mama yao

Lamar amekuwa akionyesha upendo kwa dada yake huyo mara kwa mara ikiwemo na kumtaja kwenye nyimbo zake kama ‘Keisha’s Song (Her Pain)’ alirap kwa kusema, “My little sister 11, I looked her right in the face the day that I wrote this song, sat her down and pressed play.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents