Habari

Kenya: Asimulia alivyopata Ukimwi ndani ya usiku mmoja ”Baba watoto wangu kapima kakutwa hana”

Naomi Ireri, 41, ni mwanamke anayeishi na virusi vya ukimwi kutoka nchini Kenya ambaye amejizolea sifa kutokana na ujasiri baada ya kuamua kusimulia jinsi walivyoambukizwa ukimwi.

Naomi Ireri

Bi Naomi mbali na wazi hali yake ya HIV katika vyombo vya habari nchini Kenya na hata kwenye mitandao ammeamua kuzungumzia mazingira au matukio yaliyomfanya yeye kupata Ukimwi.

Naomi ambaye kwa sasa ana mtoto wa miaka saba alifahamishwa kuhusu hali yake wakati alipokuwa na mimba ya miezi mitano wakati alipokuwa akihudhuria kliniki kabla ya kujifungua

“Nilipoenda kufanyiwa vipimo vya damu, wahudumu wa afya walichukua muda kabla ya kunipa majibu yangu, na hapo nikaanza kuwa na wasiwasi -kwanini matokeo yangu yalichukua muda hivyo”,Naomi alisema.

Baada ya muda mmoja wao alimuita Naomi na kumuuliza iwapo alikuwa amepimwa, hali yake ya ukimwi na akasema la! na hapo ndipo alipopewa habari kuwa amepatikana na virusi vya HIV.

Naomi alishituka sana na kujawa na hofu asijue la kufanya. Anasema kilichomjia akilini mwake ni kuwa baba ya mtoto wake aliyekuwa na uja uzito wake ndiye aliyemuambukiza.

Na alipompigia simu huku akilia alimweleza kuwa “umefaulu kuniambukiza Ukimwi ” alisema Naomi.

Ila mpenzi wake Naomi alikanusha hayo na kusema kuwa alikuwa tayari kupimwa virusi wakiwa pamoja.

Waliporejea hospitali matokeo ya Naomi yalitokea akiwa na ukimwi ilhali mpenzi wake hakuwa virusi.

“Nilishangaa sana ni vipi mimi nilikuwa na virusi na mpenzi wangu alikuwa hana” alisema.

”Hapo ndipo nilianza kurejesha akili yangu nyuma, ili kukumbuka mahusiano mengine ya kimapenzi niliyokuwa nayo”

Baada ya kutafakari kwa muda anasema alikumbuka mwanamume mmoja ambaye alishiriki ngono naye mara mmoja tu zamani kabla ya kukutana na mpenzi wake wa sasa.

Naomi aliendelea kusimulia kwamba aliambukizwa ukimwi mwaka wa 2010 lakini alifahamu hali yake mwaka wa 2012 kumaanisha kuwa alikutana na mpenzi wake ambaye ni baba ya mtoto wake akiwa ameambukizwa ila hakufahamu wakati huo .

Je ilikuwaje hadi akaambukizwa ukimwi?

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Naomi anasema kuwa ndoto yake ya kupata mpenzi ambaye angemchumbia hadi amuoe ilimshawishi sana, alipokutana na mwanamume mmoja mwaka wa 2010.

Kama kawaida ya mahaba anasema kuwa yalikuwa moto sana na katika kipindi cha wiki mmoja hivi mapenzi yalikuwa yamenoga sana hadi wakaamuwa kuwa wangeshiriki ngono.

Pia anasema kuwa mtu huyo alikuwa amemuahidi ndoa na mambo mengine mengi.

Baada ya wiki mmoja waliamua siku na wakati wa kukutana, anasema kuwa alitumai kuwa penzi lake na mwanamume huyo lingenoga na hatimaye wawe mume na mke.

Walikutana kama walivyokuwa wamepanga, na kushiriki naye mapenzi kwa usiku huo, baada ya hapo hakumuona tena mwanamume huyo na kila mara alipojaribu kupiga simu, alikuwa haipokei na wakati mwingi ilikuwa imezimwa.

Je ilikuwaje hadi akaambukizwa ukimwi?

“Nilisononeka sana kwa kuwa sikuweza kumfikia mwanamume huyo ambaye nilikuwa nimeanza kumpenda, ila sikujua kwake, wala sehemu ya kumtoa wala sikufahamu jamaa yeyote kutoka kwao au hata rafiki “alisema Naomi.

Baada ya muda Naomi aliamua kuendelea mbele na maisha na hata kuingia kwa uhusiano mwingine wa kimapenzi na mwanamume ambaye sasa ni baba ya mtoto wake.

Aliposhika mimba ndipo matukio ya usiku mmoja tu na mwanamume ambaye hakumfahamu vyema yalianza kumfuata kwa kuwa alifahamishwa kuwa alikuwa na virusi.

Tangu alipofahamu hali yake, baba ya mtoto wake pia alifutilia mbali uchumba wao lakini akiaahidi kuwa atamtunza mtoto akiwa mbali na wao.

Naomi alijuta sana lakini aliamua kuangazia maisha yake kama kielelezo cha jamii, kwa kujitokeza kwa umma kusimulia jinsi chaguo la kuharakisha penzi lilivyomletea ugonjwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents