Tupo Nawe

Kenya: Baba amuua mwanawe kisa majina ya cheti cha kuzali

Polisi mjini Murang’a wamemkamata Paul Njuguna Njogore mwenye umri wa miaka 25, anayedaiwa kumuua mtoto wake wa kiume, Collins Waweru mwenye umri wa miaka mitano.

Paul Njuguna Njogore anadaiwa kumuua mtoto baada ya mama kukataa kuweka majina ya baba huyo kwenye cheti cha kuzaliwa.

Mtuhumiwa inadaiwa alikwenda kwa bibi yake na mtoto huyo na kusubiria mpaka alipolala na ndipo akatekeleza mauaji hayo kwa kutumia panga.

Baba huyo alitiwa mbaroni na jeshi la polisi siku ya Jumatano ya Apirili 10, katika kituo cha biashara cha Mukarara karibu na nyumbani kwake kwenye operesheni iliyokuwa ikiongozwa na ‘Muranga East Directorate of Criminal Investigations’ (DCI), Juliana Muthini.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Murang’a Josephat Kinyua amesema mshukiwa huyo alizozana kwanza na shangazi wa marehemu ambaye alikuwa akimlea na kufanikiwa kukimbia.

“Alikatwa mkono wake wa kushoto lakini alifanikiwa kutoroka na kupiga mayowe kuwaita majirani,”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW