Habari

Kenya kuombewa

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi wa dini na kupanga siku maalumu ya maombi kwa taifa hilo kabla ya kuingia kwenye siku ya uchaguzi mkuu wa urais Oktoba 26 mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta alivyokutana na viongozi wa dini mapema leo Jumatano.

Rais Kenyatta amesema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa amekutana na viongozi hao kwa lengo moja la kuongeza nguvu ya maombi katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea uchaguzi huo.

Kenyatta amesema wamekubaliana na viongozi hao kuwa Jumapili ya tarehe 22 Oktoba, itakuwa siku maalumu kwa nchi hiyo kuombewa.

The first step —and one which I hereby call for —is an extended period of prayer and reconciliation this weekend. After consultations with religious leaders, I have reached this decision to call on all Kenyans to pray for their country in their mosques, temples and churches, culminating in a National Day of Prayer on Sunday 22nd October 2017. “ameandika Rais Uhuru Kenyatta kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo, Kenyatta amesema maombi hayo hayatakuwa kwa ajili ya taifa tu bali yatajumuisha pia na maombi maalumu kwa viongozi watakaochuana kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents