Habari

Kenya kupiga panga mishahara ya Rais na Wabunge

By  | 

Tume ya mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma nchini Kenya imetangaza kupunguza mishahara ya viongozi wakuu wakiwemo Rais na wabunge. Pia tume hiyo imependekeza kufutwa kwa marupurupu ya kipimo cha usafiri wa magari kwa magavana na wabunge.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Sarah Serem amesema  mpangilio mpya wa malipo utaokoa Sh8 bilioni (dola 80 milioni za Marekani) kila mwaka na kupunguza jumla ya mishahara inayolipwa watumishi wa umma kwa asilimia 35 na mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa Agosti 8 mwaka huu.

Kutokana na hilo sasa Rais atakuwa akilipwa Sh1.4 milioni kila mwezi badala ya Sh1.65 milioni, naye naibu wake awe akilipwa Sh1.2 milioni, Mawaziri watakuwa wakilipwa Sh924,000 , Spika wa Bunge Sh1.1 milioni, nao magavana wa kaunti Sh924,000.  Soma mchnganuo mzima hapa chini.

 • Rais: Sh1.4 milioni kutoka Sh1.65 milioni
 • Naibu Rais: 1.2 milioni kutoka 1. 4 milioni
 • Mawaziri: Sh924,000 kutoka Sh1.056 milioni
 • Makatibu wa Wizara: Sh765,000 kutoka Sh874,000
 • Magavana: Sh924,000 kutoka Sh1.056 milioni
 • Wabunge: Sh621,000 kutoka Sh710,000
 • Maspika: Sh1.155 milioni kutoka Sh1.30 milioni
 • Naibu Spika: Sh924,000 kutoka Sh1.006 milioni
 • Viongozi wa Serikali na Upinzani Bungeni: Sh765,000 kutoka 1.020 milioni
 • Madiwani (Wawakilishi wa Wadi): Sh144,000 kutoka Sh165,000
 • Mawaziri wa Serikali za Kaunti: Sh259, 875 kutoka Sh350,000

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments