Habari

KENYA: Majina na picha za wadaiwa sugu wa mikopo ya elimu ya juu kuwekwa hadharani

Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini Kenya (HELB), Inatarajiwa kuchapisha majina na picha za wale wote walioshindwa kulipa mkopo huo na kuyaweka hadharani.

Leo Jumatatu Novemba 18, 2019, Bodi hiyo imesema kwamba itachapisha majina na picha kwenye magazeti ya serikali walioshindwa kulipa madeni hayo tangu 1975.

Baadhi ya walionufaika na hawajalipa hawakuitikia wito wetu wa awali na hivyo kusababisha wanachuo wengine wanaohitaji mikopo kukosa huduma hiyo,” Imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, HELB imesema kuwa itachapisha majina na picha zao baada ya siku 30 na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Walionufaika na mkopo huo ambao hawajaanza kulipia wanashauriwa kuwasiliana na HELB kuhusu akaunti za mikopo yao, na watakaokuwa wameshindwa kulipa ndani ya kipindi hicho majina na picha zao tutaziweka magazetini,” Imeeleza taarifa hiyo.

Bodi hiyo imesema jumla ya watu 85,000 walionufaika na mkopo huo hawajalipa na wanadaiwa Ksh. bilioni 52.1 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents