Burudani ya Michezo Live

Kenya: Mchungaji azua gumzo kwa maneno yake ”Ifikapo mwezi wa sita” (+Video)

Mchungaji mwenye umaarufu mkubwa nchini Kenya, James Ng’ang’a amezua gumzo baada ya kudai kuwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu 2020 atakuwa na uwezo wa kumwachisha kazi mtu yoyote serikalini kwa kutaja jina lake tu.

Kipande cha video kimekuwa kikienea mtandaoni akionekana, Mtumishi huyo wa Mungu akitoa kauli hiyo ambayo imezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

”Kufikia mwezi wa sita, nitakuwa na uwezo hata wa kumfuta mtu kazi serikalini mimi Ng’ang’a, Sitatangaza nitakuwa nasema tu wewe uwende nyumbani na anakwenda, ninyi nitakuwa nikiwaambia lakini sitatanga kwenye Tv,” amesema mtumishi huyo wa Mungu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW