Burudani ya Michezo Live

Kenya: Mvuvi aokolewa kwa helkopta katika mafuriko

Mvuvi mmoja amenusuriwa kutoka katika kisiwa ambacho alikuwa amekwama tangu siku ya Ijumaa kutokana na mafuriko makubwa.

Image result for Jinsi mvuvi huyu wa Kenya alivyookolewa na ndege katika mafuriko

Vincent Musila alikuwa amekwenda kuvua samaki kama kawaida katika mto mmoja mjini Thika katikati mwa Kenya wakati mto huo ulivyovunja kingo zake.

Watu wengi walitazama bila usaidizi wowote walipokuwa wakisubiri usaidizi wa dharura ili kumuokoa.

Zaidi ya watu 250 wameuawa na wengine milioni kuathiriwa na mafuriko na maporomoko katika eneo lote la Afrika mashariki.

View this post on Instagram

———————————————————————-Mjini Thika katikati mwa Kenya mvuvi mmoja jina lake Vincent Musila ameokolewa na Helikopta ya Polisi baada ya kukaa zaidi ya ziku mbili kwenye kisiwa huku akizungukwa na maji pande zote. Kutokana na mafuriko yanayoendelea katika maeneo hayo kingo za mtu aliokuwa anatarajia kuvua mvuvi huyo zilivunjika na kusababisha maji kuzagaa kwa wingi. Takribani watu 250 wanaripotiwa kufariki na wengine zaidi ya Millioni wameathirika kutokana na mafuriko maeneo yote ya Afrika mashariki. Vincent Musila, alikuwa akienda kuvua kama ilivyokuwa kazi zake za kila siku lakini muda mchache baadae akaona maji yanamzingira na anashindwa kuvuka. Majirani wa eneo hilo waliendelea kufanya jitihada za kumuokoa ikiwa ni pamoja na kumrushia kamba zoezi ambalo halikufanikiwa kumuokoa Bwana Musila. Musila alieleza chombo kimojawapo cha habari nchini Kenya kuwa hali ilikuwa mbaya zaidi wakati wa usiku, ambapo alipambana na wanyama kama Mamba, Kiboko na mbu walimsumbua sana. Source: Citizentv. Written and edited by @yasiningitu

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Takriban nusu ya vifo 120 vimetokea nchini Kenya huku zaidi ya watu 160,000 wakiathiriwa.

Bwana Musila anasema kwamba mafuriko hayo yalianza ghafla kutoka katika eneo moja lililiopo katikati ya mto huo , nje ya mji wa Thika.

”Sekunde chache baadaye kulikuwa na maji kila mahali nikashindwa kuvuka”.

”Hali imekuwa mbaya katika kipindi cha siku tatu katikati baridi na mvua. Nilikuwa na njaa na nilifikwa na mambo mengi”.Vincent Musila akilaChakula cha kwanza cha Vincent Musila baada ya siku tatu

“Kulikuwa na mbu chungu nzima na nilikuwa nikiogopa wanyama kama vile mamba na kiboko . lakini nafurahi na najihisi vyema baada ya uokoaji huo.

Nahisi kana kwamba nimezaliwa upya, aliambia chombo cha habari cha NTV nchini Kenya”.

Image result for Jinsi mvuvi huyu wa Kenya alivyookolewa na ndege katika mafuriko

Makundi ya watu waliokongamana kandokando ya mto huo walifurahia wakati ndege aina ya helikopta ya maafisa wa polisi ilipowasili kumnusuru,

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kwamba baadhi ya raia hao walimchukua manusura huyo na kumpeleka katika mkahawa ambapo alikula viazi karanga na sausage – ikiwa ni chakula chake cha kwanza katika kipinid cha siku tatu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW