Habari

KENYA: Mwili wa mtu mmoja na gari lake lililozama baharini waopolewa Mombasa – Video

KENYA: Mwili wa mtu mmoja na gari lake lililozama baharini waopolewa Mombasa - Video

Mwili wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini katika kivuko cha likoni mjini Mombasa mapema siku ya Jumamosi umeopolewa. Shirika la hudumu za Ferry nchini Kenya KFS limesema kwamba gari la John Mutinda lilishuka katika mreremko kwa kasi ya juu. Kisa hicho kinarejesha upya kumbukumbu za mkasa mwengine mwezi Septemba mwaka huu ambapo Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walikufa maji.

Iliwachuku waokoaji takriban siku 13 kuopoa miili pamoja na gari walilozama nalo.

Taarifa ya KFS kuhusu kifo cha Mutinda ilisema: Dereva alikuwa akiendesha gari aina ya saloon ambaye nambari zake za usajili hazijafichuliwa baada ya kununua tiketi aliteremka kwa kasi katika mteremko wa feri na kuingia baharini.

Shirika hilo liliongezea kwamba dereva huyo alikataa kusimamisha gari hilo licha ya juhudi kadhaa za maafisa wa feri kumsimamisha.

Maboti ya uokoaji ya KFS , wanamaji wa Kenya Navy na maafisa wa polisi wakishirikiana na waokoaji wengine yalifika katika kivuko hicho mara moja na kuanzisjha operesheni ya kulisaka gari hilo mara moja.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho mapema alikuwa amesema kwamba serikali ya kaunti hiyo ilikuwa imepeleka kitengo chake kushirikiana na wakojia wengine wa idara tofauti za serikali.

Jinsi kisa cha Maryam Kighenda na mwanawe lilivyojiri:

Sept 29: Gari dogo aina ya soloon lililoarifiwa kuwa na watu wawili ndani lazama katika kivuko cha Likoni

Sept 30: Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ferry Bakari Gowa asema kwamba wataalam wamebaini kuwa gari hilo lilizama kima cha mita 60, hivyobasi kufanya kuwa vigumu kuliokoa.

Sept 30: Shughuli za uokoaji ambazo zimejumuisha maafisa kutoka vitengo vya Kenya Navy, Kenya Ferry, na wapiga mbizi wa kibinafsi zaanza.

Okt 1: Kivuko cha feri chafungwa kwa saa tatu ili kuruhusu utafutaji ulioendelea wa gari na miili ya waliokuwemo ndani.

Okt 2: Familia ya waathiriwa yalalamikia kujikokota kwa operesheni ya uopoaji miili ya waathiriwa.

Okt 2: Kikosi cha pamoja katika operesheni ya uopoaji kinasema kimegunuda sehemu lilipo gari. Hii ni baada ya kuyakagua maeneo kadhaa yalioshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 3: Maafisa wanaendelea kushughulika na ukaguzi wa maeneo yalioshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 7: Wapigambizi wa Afrika Kusini wajiunga katika operesheni hiyo ya uopoaji.

Okt 8: Wapigambizi waanza kazi ya kutafuta miili na gari.

Okt 9: Gari lililokuwa limezama katika kivuko cha Likoni limeonekana. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna asema haiwezi kuthibitishwa iwapo ndilo gari lililozama Jumapili Septemba 29.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents