Habari

Kenya: Othuol wa Churchill Show kuzikwa October 24, Tsh Milioni 21 kugharamia mazishi yake

Taarifa kutoka kwa katibu wa kamati ya sanaa ya ucheshi Ken Waudo, inasema kua mipango ya mazishi ya mchekeshaji wa Churchill Show Ben Maurice Onyango aka Othuol Othuol inakadiriwa kuchangisha kiasi cha pesa chenye kima cha million moja (1m) ya Kenya ambayo ni sawa na tsh 21, 377, 862. 72

Othuol alifariki juzi kwenye hospitali kuu ya Kenyatta, alipokimbizwa ilikupata matibabu ya dharura baada ya kuzimia nyumbani kwao Kitengela.

Othuol amekua akiugua ugonjwa wa kifua kikuu na tena maradhi ya uvimbe kwenye ubongo. Mazishi yake yamepangiwa kufanyika Octoba 24 nyumbani kwao Ndere, Alego kwenye jimbo la Siaya.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents