Burudani ya Michezo Live

KENYA:Walimu na wanafunzi wapelekwa hospitalini kwa kuathiriwa na kemikali – Video

Walimu na wanafunzi wapelekwa hospitalini kwa kuathiriwa na kemikali - Video

Wanafunzi na walimu kadhaa nchini Kenya wamefikishwa hospitalini baada ya kemikali hatari iliyokuwa ikitumiwa wakati wa mtihani wa vitendo wa Kemia wa shule ya sekondari kuwaathiri.

Mwanafunzi mmoja alipata majeraha makubwa ya kuungua usoni wakati wa mtihaniwa vitendo huku wengine walifikishwa hospitalini baada ya kupata kizunguzungu.

Apolli Otieno alikuwa akichemsha kemikali ya aina ya Xylene kuchunguza matokeo yake katika maabari ya shule ya sekondari ya Kajulu, mjini Kisumu, ilipolipuka na kuchoma uso wake, Gazeti la Daily Nation liliripoti.

Kemikali iliyolipuka ilitumika badala ya cyclohexane baada ya wizara ya elimu kutoa maagizo hayo.

Kaimu mwenyekiti wa Baraza la mitihani nchini Kenya Mercy Karogo alitoa maelekezo tarehe 1 mwezi Novemba kununua kemikali ya Xylene mbadala wa cyclohexane. Pia wakuu wa shule walielekezwa mahali pa kununua kemikali hiyo.

”Hii ni kuwataarifu kama kuna ugumu katika kupata kemikali ya cyclohexane, unashauriwa kupata xylene kama mbadala. Hii inapatikana katika kampuni ya Kobian Kenya Ltd au kwa wasambazaji wengine wa kemikali hiyo,” ilieleza taarifa hiyo.

Msambazaji wa bidhaa hiyo alimuandikia Bi Karogo akiomba kutoa maelezo kwa wakuu wa shule kuhifadhi kemikali hiyo kwenye chupa ya kioo.

”Tumesikia kuwa wasambazaji wengine wanapakia kemikali kwenye chupa za plastiki. Xylene ni huyeyusha plastiki. Tuna xylene ya kutosha kwenye chupa za kioo,” barua pepe yenye kichwa cha ujumbe ”haraka” uleleza.

Gazeti la The Standard liliripoti kuwa mwalimu alikimbizwa hospitali katika kaunti ya Trans Nzoia bada ya kuugua wakati wa mtihani huo wa vitendo.

Chama cha walimu kimeviambia vyombo vya habari kuwa wanafunzi kadhaa na walimu walikuwa wakipata matibabu baada ya kulalamika kuwa wana kizunguzungu baadhi walianguka wakati wa mtihani wa vitendo.

Serikali ya Kenya imekeana kuwa kemikali iliyotumika katika mtihani ilikuwa na sumu na kusema kuwa ”kemikali nyingi zinazotumika katika masuala ya kemia ni hatari, na kuwa xylene si hatari kama ilivyo kemikali ya Chlorine na Bromine.

BBC ilipowasiliana na wizara kwa ajili ya kuzungumzia kuhusu mwanafunzi aliyeungua, waziri Belio Kipsang hakupatikana. Awali alieleza kuwa hakujakuwa na malalamiko rasmi kuhusu tukio la mwanafunzi huyo.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW