Habari

Kenya watangaza visa vipya 22 vya corona, sasa wagonjwa ni 81

Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema jumla ya watu 22 kati ya 300 waliopimwa wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona na hivyo kufanya idadi ya wagonjwa wa Covid 19 nchini humo kufikia 81.

Katika hatua nyingine Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameomba radhi kwa wananchi wake kufuatia kitendo cha Askari wa Jeshi la Polisi nchini humo kutumia nguvu kubwa kuwatawanya wananchi waliokutwa nje baada ya katazo la kutotoka nje kuanzia saa 1 usiku hadi saa 11 alfajiri kuepuka maambukizi ya corona.

Afrika Kusini imechukua sampuli za watu 42,500 kwa ajili ya kupima virusi vya corona, ikiwa ni sampuli nyingi zaidi Afrika. Nchi hiyo tayari imethibitisha wagonjwa 1,353 wa corona.

Misri imerekodi vifo 46 vya covid-19 hadi sasa.

Watu 10 wamepona corona Cameroon.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents