Afya

Kenya yatangaza idadi kubwa ya vifo vya Corona kwa siku

Idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa corona Kenya inakaribia 300 kulingana na takwimu zilizotolewa na serikali Jumanne.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kwamba watu wengine 14 wamefariki kutokana na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24 na hivyobasi kufanya idadi ya waliofariki kufikia sasa kuwa 299.

Aidha idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maradhi hayo imefikia 18,581 baada ya waziri wa Afya kutangaza wagonjwa wengine 606.

Kati ya wagonjwa hao wapya 583 ni raia wa Kenya huku 23 wakiwa raia wa kigeni , wanaume wakiwa 409 nao wanawake wakiwa 197.

Mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi minne huku mtu mwenye umri mkubwa zaidi akiwa mzee wa miaka 85

https://www.youtube.com/watch?v=WQ8zYCid66I

https://www.youtube.com/watch?v=SH5JldIkjdQ

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents