Habari

Kenya yazima simu bandia zaidi ya milioni moja

Kwa mara ya kwanza jana zaidi ya simu milioni moja za bandia nchini Kenya ziligeuka ‘makopo’ baada ya kuzimwa na tume ya mawasiliano ya nchi hiyo, CCK.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa CCK Francis Wangusi alisema Airtel imeziondolea mawasiliano simu 740,000, Safaricom 680,000, wakati mtandao wa Orange ukizipiga chini simu 75,000.

Pia serikali imesema ina mpango wa kuondoa kodi kwenye simu ili kuzifanya simu halali ziweze kuwa na bei nafuu ambazo wananchi wa Kenya watazimudu.

CCK imesema idadi ya simu bandia inaweza kuwa chini ya milioni 2.5 tofauti na ilivyokuwa imekadiria mwanzo na kuongeza kuwa wananchi wengi wa nchi hiyo walikuwa wameshanunua simu halali.

“Wale ambao simu zao bado zinafanya kazi na ni bandia wasisherehekee kwasababu nazo zitazimwa na ni kwa maslahi ya nchi hii,” alisema Wangusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents