Habari

Yajiyojiri kwenye kesi ya Kitilya na wenzake

Kesi ya aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, Harry Kitilya, aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanbic tawi la Tanzania, Miss Tanzania 1996, Shose Sinare pamoja na mwenzao Sioi Solomoni imesikilizwa leo.

images-Miss_696029087

Kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Jumanne hii katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam lakini imeahirishwa hadi Mei 18 kutokana na jalada la kesi hiyo ambalo lilitegemewa kurudi leo kutorudishwa. Watuhumiwa wamerudishwa tena rumande.

Aidha watuhumiwa walitakiwa kufika mahakama kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya kufika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani hiyo May 5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents