Burudani

Oscar Pistorius kuendelea kukaa jela zaidi

Bodi ya parole nchini Afrika Kusini jana ilisogeza mbele kutolewa jela kwa Oscar Pistorius anayetumikia kifungo kwa kumuua mpenzi wake.

140317-oscar-pistorius-trial-11a_0e1311e12dff9296d3e0ff6795d39191

Bodi hiyo ilikutana jijini Durban mwezi uliopita lakini iliahirisha tena kesi yake kwa wiki mbili. Katika kipindi hicho idara ya haki ilisema haikupata muda wa kumaliza kesi ya Pistorius kutokana na kuwa na mambo ya kuyapitia.

Haijatangazwa lini bodi hiyo itakaa tena kusikiliza upya uamuzi wa parole.

Mwanariadha huyo mlemavu alifungwa mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake huko Pretoria kwenye Valentine’s Day, mwaka 2013. Hadi sasa ameshakaa jela kwa mwaka mmoja.

Awali alikuwa aachiliwe August 21 kuendelea na kifungo cha ndani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents