Habari

Kesi ya ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’ zasubiriwa nyaraka kutoka Australia

Kesi inayomkabili Shaban Hussein (Ndama mtoto wa Ng’ombe) ya makosa matano imehairishwa mpaka 12/2/2018. Wakati wa kusikiliza kesi hiyo upande wa mshtakiwa umedai unasubiri nyaraka kutoka nchini Australia ziweze kuwasilishwa.

Wakili wa Serikali, Estazia Wilson amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa wameshapeleka maombi ya nyaraka za kesi hiyo (Foreigner Affairs). Kutokana na hatua hiyo, Wakili wa utetezi Jeremiah Ntobesya aliomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Makosa anayokabiliwa Ndama inadaiwa February 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka za kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha mabox manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

March 6, 2014, Dar es Salaam, anadaiwa kughushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents