Michezo

Kesi ya Oscar Pistorius kuendelea hadi May 16

Kesi ya mauaji ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeongezwa muda na sasa itasikilizwa hadi May 16 kwenye mahakama kuu ya Pretoria.

Oscar Pistorius in court

Pistorius alimpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwenye Valentine’s Day mwaka jana. Pistorius anajitetea kuwa alidhani Reeva alikuwa kibaka aliyeingia ndani mwake japo serikali inadai hayo yalikuwa mauaji ya kudhamiria ambayo ameyakana.

Kesi hiyo itakuwa na tarehe 7 na 11 April na itaendelea tena April 14 hadi May 16. Hivi karibuni Pistorius alipanga kuliuza jumba lake kifahari la Pretoria ili kulipa gharama za mawakili.

Kesi hiyo inaendelea Jumatatu hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents