Habari

Kesi ya Scorpion yapigwa kalenda

Kesi ya inayomkabili Salum Njwete, maarufu ‘Scorpion’ ya unyang’anyi kwa kutumia silaha imeahirishwa hadi Mei 2 mwaka huu, kufuatia shahidi namba nane kwenye kesi hiyo kushindwa kufika mahakamani hapo.

Kesi hiyo iliahirishwa Jumanne hii na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Flora Haule, kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Cheses Gavyiole, baada ya Deus Magosa (45), ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ya kumjeruhi kwa kumtoboa macho Saidi Mrisho, kushindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na sukari.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga,alisoma maelezo ambapo kuna baadhi shahidi huyo alikiri kuyatoa Polisi na mengine kuyakana na kudai kwamba askari alimchukulia maelezo mara mbili, hatua ambayo iliilazimu mahakama hiyo kuahirisha kusikiliza ushahidi huo hadi Aprili 18 (Jumanne hii).

Inadaiwa kwamba Septemba 6, mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Njwete alimjeruhi Said Mrisho na kumuibia Cheni na fedha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents