Michezo

Kesi ya Simba na Yanga inayomhusu Hassan Kessy yaahirishwa

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15, 2016.

KESSY-640x5681-640x568_2

Simba imelalamika mbele ya kamati hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa, mchezaji Hassan Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo yenye mashakani yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu katika tarehe itakayopangwa hapo baadaye. Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kutotimia kwa adadi ya wajumbe wa kamati nzima. Idadi ni lazima wajumbe zaidi ya watatu wathibitishe kushiriki.

Ilikuwa isikiliwe Jumapili baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba ikiilalamikia Klabu ya Young Africans, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati bado ana mkataba na klabu Simba.

Shauri la Simba dhidi ya Young Africans lilishindika kusikilizwa kwa sababu Young Africans hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi.

Kama hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja. Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo baadaye ni pamoja na yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati lakini wakashindwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents