Burudani

Kesi ya Usher Raymond yafika patamu

Huenda kesi inayomuandama mwanamuziki Usher Raymond, ikafutwa wakati wowote endapo tu jaji wa mahakama akiridhia ombi lililotolewa na mwanasheria wa msanii huyo juu ya kutokumwambukiza mtu ugonjwa wa zinaa.

Usher Raymond alishutumiwa kumuambukiza ugonjwa wa zinaa mrembo Quantasia Sharpton. Kupitia mwanasheria wa mrembo anayedai kuambukizwa ugonjwa huo Lisa Bloom, aliiomba mahakama kumlazimu msanii huyo amlipe mteja wake fidia ili aweze kujitibu ugonjwa alioupata kutokana na kujamiia naye.

Hata hivyo mwanasheria wa msanii huyo amepinga madai hayo na kusema kuwa mteja wake hana na hajawahi kuwa na ugonjwa wowote wa zinaa na ni mtu anayejali afya yake kwa kuzingaztia matumizi mbalimbali ya kinga kabla ya tendo.

Pia zimeeleza kuwa kama msanii huyo hakuwa na ugonjwa wa zinaa hivyo basi huwenda mrembo huyo alikuwa nao na alitaka kumuambukiza Usher.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents