Habari

Kesi ya vigogo TRL kuanza kusikilizwa

Kesi inayowakabili vigogo 11 wa Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mabehewa 25, inatarajiwa kuanza kusikilizwa Desemba 5, mwaka huu.

2-2

Kesi hiyo iliwasilishwa Jumatatu hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa awali.

Wakili kutoka aasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Magala Ndimbo, akisaidiana na Max Ally, alidai mahakamani kwamba walikuwa tayari kwa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

Wakili wa utetezi, Ambrose Malamsha, aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu maelezo wamepewa baada ya kuingia mahakamani na washtakiwa wawili hawana wawakilishi.

Hakimu Nongwa alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 5, mwaka huu, mawakili wa washtakiwa wanatakiwa kuwepo.

Vigogo hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu, Mkuu wa Kitengo cha Makenika na Mhasibu Mkuu Jasper Kisiraga, Kaimu Meneja wa Usafiri, Mathias Massae, Kaimu Mhandisi wa Ufundi na Meneja Ujenzi, Muungano Kaupunda na Mkuu wa Ufundi na Meneja Ujenzi, Ngoso Ngosomwiles.

Wengine ni Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Paschal Mafikiri, Mhandisi Mipango Kedmo Mapunda, Kaimu Mhandisi wa Mawasiliano, Felix Kashaingili, Mkuu wa Usafiri wa Reli, Lowland Simtengu; Mkuu wa Ubunifu na Utengenezaji wa Nyaraka, Joseph Syaizyagi na Kaimu Mkuu wa Usafirishaji; Charles Ndenge.

Katika hati ya mashtaka inadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi 2013 na Juni 30, 2014, katika Makao Makuu ya TRL, Kisamfu akiwa mfanyakazi wa mamlaka hiyo, alitumia vibaya madaraka yake kwa kushindwa kusimamia vizuri zabuni kama ilivyokuwa inatakiwa kwenye vigezo na masharti.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: MTANZANIA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents