Michezo

Kesi ya viongozi wa TFF, jopo la mawakili 5 wajipanga kushinda kesi (Video )

Mmoja kati ya jopo la mawakili watano wanaosimamia kesi ya viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,TFF, Jerome Msemwa amesema watahakikisha wateja wao wanakuwa huru kwa kupatiwa dhamana juu ya mashitaka wanayo yakabili.

Wakili, Jerome Msemwa akizungumza na vyombo vya habari mahakamani Kisutu

“Mahakama itatoa tafsiri ya kisheria je, wakati kesi imeanza kusikilizwa, upande wa upelelezi unaweza ukaomba na ukapewa ruksa ya kupeleleza kesi wakati washitakiwa wapo mahakamani na kwa sheria hipi, ndio mahakama itakuja kulitolea ufafanuzi swala hilo ?, kwa washitakiwa kukamatwa kufikishwa mahakamani na halafu wanaomba tena upelelezi wakesi wakati swala lipo mahakamani.

Rais wa TFF,Jamal malinzi(katikati), makamu wa klabu ya Simba,Geofrey Nyange ‘Kaburu’(kulia) na katibu Mkuu wa TFF,Mwesigwa Celestine (kushoto)

 

“Na pointi yetu ya pili ni maombi ya dhamana, mahakama hii tumeiomba itoedhamana kwa wateja wetu kwasababu tunaamini kwamba kunasheria ya bunge inayokataza dhamana na kunakatiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana kwahiyo vituviwilivitakuja kuamuliwa siku ya Jumatatu ya tarehe tatu mweziwa saba” amesema wakili Jerome Msemwa.

Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva,(kulia) makamu wake,Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (wapili kutoka kulia) Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine (wamwishokushoto) na ,rais TFF, Jamal malinzi (wapili kutoka kushoto) wakiingia mahakamani leo

 

Naye wakili Msomi Aloyce Komba amesemakuwa hojawalizotoa ni katika kuhakikisha haki inatendeka

“Tumetoa hoja zinazozingatia haki inatendeka na inaonekana kutendeka iliwateja wetu kwa mashitaka waliyoshitakiwa yaanze mara moja na yaishenawao wapate hakizaozigine ikiwemo haki ya dhamana tuliyoiomba. Natumesema mashitaka yotetukiyaangalia ni ya kugushi kugushi ingawa mengine kama matatu wameyabadilisha yakawa ya kutakatisha fedha ilitu wakose dhamana” amesema wakili Msomi Aloyce Komba.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine walitiwa nguvuni siku ya Jumanne mchana na kufikishwa mahaka ya hakimu mkazi Kisutu leo kwa lushitakiwa na makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha hivyo mahakama imeamuru kupelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea hadi Jumatatu ya Julai 3 kesi yake itakaposikilizwa tena.

Jopo la mawakili watano likiongozwa na Jerome Msemwa, wakili Msomi Aloyce Komba, James Bwana, Komba na wakili Mpedule ndio wanaosimamia kesi ya viongozi hao wa ngazi ya juu ndani ya shirikisho kuhakikisha nawakuwa huru kama wenyewe walivyoeleza.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents