Michezo

Kevin De Bruyne kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita

Mchezaji wa Manchester City, Kevin de Bruyne, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia goti siku ya Jumatano.

30A48E6400000578-0-image-a-15_1453995799845

De Bruyne alipata jereha la goti la kulia katika mchezo wa kombe la Capital, ambapo Man City, waliwakabali Everton, na kushinda kwa mabao 3-1.

30AA169D00000578-3421206-Manchester_City_playmaker_Kevin_De_Bruyne_left_the_Etihad_Stadiu-m-32_1453996166868

Wakala wa mchezaji huyu Patrick de Koster, amesema, “Nimezungumza na Kevin, amesema atarudi uwanjani kwa nguvu zaidi.”

Mchezaji huyo atakosa michezo muhimu ya timu yake ukiwemo ule wa fainali ya kombe la Capital, dhidi ya Liverpool, hapo Februari 28, pia atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Dynamo Kiev.

Kulikua na wasiwasi huenda mchezaji huyo asingeweza rudi dimbani mpaka mwisho wa msimu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents