Kevin Durant ajiwekea historia NBA

Mshambuliaji wa timu ya mpira wakikapu ya Golden State Warriors, Kevin Durant amefanikiwa kushinda jumla ya mabao 20,000 toka kuanza tasnia ya mchezo huo na kufanikiwa kufikisha alama hizo wakati wa robo ya pili walipocheza dhidi ya LA Clippers siku ya Jumatano licha ya kufungwa kwa jumla ya vikapu 125-106 nakumfanya kuwa wapili NBA mwenye umri mdogo kufikia alama hizo baada ya LeBron James.

Durant amefanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kurejea Uwanjani toka alipopata matatizo na kuikosa michezo mitatu.

Akionekana kuwa mwenye hisia kubwa awapo Uwanjani, Durant alifanikiwa kuondoka na jumla ya mabao 40 usiku huo.

Amekuwa miongoni mwa wachezaji watano waliyowahi kufikisha pointi hizo wakiwa hawajavuka umri wa miaka 30, akiwemo Wilt Chamberlain, James, Kobe Bryant na Michael Jordan.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW