Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Keyshia Cole akutana na rungu zito la Mahakama

By  | 

Majanga mapya yamemkumba Keyshia Cole. Muimbaji huyo ametakiwa na Mahakama kumlipa mwanamke moja kiasi cha dola 100,635 ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 200 kwa fedha za Kitanzania.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Keyshia ametakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kama fidia kwa mrembo huyo aliyefahamika kwa jina la Sabrina Mercadel ambaye alimshambulia mwaka 2014 katika makazi ya rapper Birdman mjini Los Angeles.

Msanii huyo ambaye alikuwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Birdman katika kipindi hicho, alimshambulia Sabrina baada ya kumkuta akiwa nyumbani kwa Birdman akihisi alikuwa ni mpenzi wake mwingine.

Awali Sabrina alidai kuwa alipoteza matumizi ya kidole pamoja na kukwauzwa usoni na kucha katika shambulio hilo na aliomba kulipwa kiasi cha dola 4,000,000 kutoka Cole.

Hata hivyo Cole na Birdman waliachana baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW