Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Khalighraph Jones akana kujipiga ‘Kitaulo’

Msanii  kutoka nchini Kenya, Khalighraph Jones amekanusha uvumi uliyokuwa umeenea katika mitandao ya kijamii kuwa anajichubua.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Nataka Iyo Doh’, ameiambia Radio Maisha (Kenya) kuwa kitu hicho hakipo na waliyokuwa wanaeneza uvumi huo ni watu wasiompenda lakini hiyo ilikuwa kama nafasi ya kuzidi kusonga mbele.

“Kuna image fulani watu walikuwa wamenizoea nayo na waliponiita pale The Trend nifanye interview hiyo siku nili-appear kwa different kidogo kushinda walivyokuwa wamenizoea na kulikuwa na make-up kidogo inafanywagwa, sasa ile light inakuwaga pale  kuna namna inaangaza, inakuwaga hivyo yaani mimi huwa hata sijaribu kujitetea kama ndivyo watu waliamua hivyo basi iwe hivyo” alisema.

“Ukiwa msanii especially mzee kama mimi ambaye nina fans wengi kuna watu hawanipendi, kuna watu wengine wapo kwa media hawanipendi kwa sababu Khalighraph ametokea ametengeneza pesa, ameinuka na time ile hiyo kitu ilitokea walijua hiyo ndiyo opportunity ya kunimaliza na kufunikia carrier yangu lakini hawajui mimi ni O.G, hiyo ndio platform wananipatia Mungu anazidi kuniinua juu” ameongeza.

Rapper Khalighraph Jones tayari ameshafanya kazi na wasanii wa Bongo kama Rosa Ree, Rayvanny na Christian Bella.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW