Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Khaligraph Jones atoa sababu ya kuchelewa kutoka kwa wimbo aliomshirikisha Ice Prince

Rapper hatari kutoka Kenya, Khaligraph Jones amefunguka sababu za kuchelewa kutoka kwa ngoma yake aliyomshirikisha Panshak Zamani maarufu kama Ice Prince wa Nigeria.

Akiongea na mtangazaji Teddy Agwa wa Msetoea ya Radio Citizen, Khaligraph amesema sababu za kuchelewa kutoka kwa wimbo huo ni kutokana na matatizo yaliyokuwepo kwenye uongozi wake lakini mambo yote yamekamilika na hivyo mwakani ndio itatoka.

“I believe nimeinclude kwa hiyo response ya pili lakini kama nilivyosema kulikuwa na ishu kadhaa za menejimenti kidogo, lakini zimeshamalizwa tunaamini 2018 ndio hiyo hiyo kazi itaweza kutoka,” amesema rapper Jones.

Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Omollo’ ambao umetayarishwa na Aress 66.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW