Burudani

Khloe Kardashian na mpenzi wake Tristan Thompson waweka wazi jina la mtoto wao

By  | 

Khloe Kardashian na mpenzi wake Tristan Thompson wameweka wazi jina la mtoto wao wa kwanza wa kike.

Mtoto huyo ambaye amezaliwa Ijumaa ya wiki iliyopita amepewa jina la True Thompson. Hiyo inaendeleza mishangao mingi kwa watu kutokana na majina ambayo wamekuwa wakipewa wajukuu wa familia ya Kardashians.

Khloe amethibitisha hilo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameandika, “Our little girl, True Thompson, has completely stolen our hearts and we are overwhelmed with LOVE.”

“Such a blessing to welcome this angel into the family! Mommy and Daddy loooooove you True!,” ameongeza. Hata hivyo mahusiano ya Khloe na Thompson yanadaiwa kutokuwa mazuri kutokana na mchezaji huyo kikapu wa Cleveland Cavaliers kudaiwa kumsaliti mpenzi wake.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments