Habari

Kiasi kikubwa nchi yetu inakabiliwa na jangwa – Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani amesema kuwa kwa takwimu zilizopo zaidi ya 60% ya ardhi yetu inatishiwa na hali ya jangwa.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani inayoongozwa na Ofisi yake amesema kuwa jukumu la kupanda na kutunza miti ni jukumu la Watanzania wote na si Dodoma Pekee.

‘Kwa kiasi kikubwa nchi yetu inakabiliwa na jangwa. Kwa takwimi zilizopo zaidi ya 60% ya ardhi yetu inatishiwa na hali ya jangwa. Akina mama, serikali yenu inawategemea sana katika ukombozi wa kijani,’ amesema Samia.

‘Jukumu la kupanda na kutunza miti ni jukumu la Watanzania wote. Kila mmoja wetu akiazimia kupanda na kutunza miti, Dodoma na Tanzania kwa ujumla itakuwa ni nchi pekee ya kukimbilia.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents