Michezo

Kibarua kizito SportPesa Super Cup kuanza kesho

Hii leo ni mapumziko ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kushuhudia timu kadhaa kutinga hatua ya nusu fainali huku baadhi zikiyaaga mashindano hayo makubwa na yenye mvuto wa kipekee.

Mashindano hayo yalioanza kutimua vumbi rasmi siku ya jumatatu ya tarehe 5 ya wiki hii , wadau wa soka wameshuhudia timu za Tanzania zikishindwa kufanya vyema katika michuano hiyo.

Wachezaji wa klabu ya Dar Young Africans ya Tanzania

Miongoni mwa timu zilizoyaaga mashindano haya mapema tu ni klabu ya Singida United, Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar, Tusker ya Kenya pamoja na  Simba SC ya Tanzania.

Wachezaji wa klabu ya  Nakuru All Stars ya nchini Kenya

Klabu zilizopata nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup ni Dar young Africans, Gor Mahia ya nchini Kenya, AFC Leopard ‘Ingwe’  pamoja na Nakuru All Stars zote hizi kutoka nchini  Kenya

Wachezaji wa klabu ya AFC Leopard  wakiwa katika mchezo wa dhidi ya Singida United wakicheza  kombe la SportPesa Super Cup

Michezo ya hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup  inatarajiwa kuanza kutimua vumbi  Alhamisi hii, kwa kuzikutanisha timu ya Dar Young African dhidi ya AFC Leopards na  huku Nakuru All Stars ikikabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Gor Mahia zote hizi kutoka Kenya.

Wachezaji wa klabu ya Gor Mahia wakipeana mikono na wachezaji wa Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar katika mchezo wa ufunguzi wa SportPesa Super Cup

BY HAMZA  FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents