Tupo Nawe

Kiboko wa Ajax, Jose Mourinho aipa mbinu Tottenham za kuibuka na ushindi Champions League

Aliyekuwa meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ametoa mbinu zitakazo weza kuisaidia Tottenham kuweza kuiua Ajax inayoonekana tishio kwenye michuano ya mikubwa kabisa ya Champions League.

Mourinho ametoa mbinu hizo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari kwenye mahojiano yake na kituo cha luninga cha RT Sports kuwa ni kwa namna gani Ajax anaweza kufungwa.

Jose Mourinho has given Tottenham some advice on how to beat Ajax ahead of their semi-final

Ajax imekuwa timu ambayo imewashangaza wengi kutokana na kuwapiga mabingwa watetezi wa Champions League, Real Madri na kuwafungisha virago kwenye hatua ya 16 bora huku ikifanya hivyo kwa miamba ya soka ya Italia klabu ya Juventus yenye mchezaji bora kabisa duniani Cristiano Ronaldo kwenye hatua ya robo fainali na kufanikiwa kuingia nusu fainali ambapo itacheza na Tottenham ya Uingereza.

Baada ya vijana wa Mauricio Pochettino kufanikiwa kutinga hatua ya nusu faina kwa kuwafunga wababe wa Premier League Manchester City sasa wapata ushauri kutoka kwa Mreno huyo ambaye ameitumikia Manchester United kwa mafanikio.

Ikumbukwe kuwa Mourinho, aliweza kuiyongoza Manchester United kuifunguka Ajax kwa jumla ya mabao 2 – 0 mwaka 2017 kwenye mchezo wa fainali ya Europa League na kutwaa kombe hilo huku ikifanikiwa kushiriki Champions League moja kwa moja.

Mourinho's Manchester United team beat a similar Ajax side in the 2017 Europa League final

Mreno huyo anaamini anayo fumla itakayoweza kuwazuia vijana hao wa Erik ten Hag ambao wanaonekana wapo moto kwa kuwatoa Real Madri na Juventus.

Akizungumza na RT Sport, Mourinho amesema mbinu walizotumia na kuweza kuwafunga huku akimini kuwa kama Spurs watatumia wataibuka na ushindi.

”Sisi tuliwapatia mchezo ambao wao hawakuhitaji, (tulicheza tofauti na vile walivyohitaji wao tucheze), wakalalamka namna tulivyojijenga, walimlalamikia Marouane Fellaini, walilalamika kwasababu hawakuweza kuendana na namna tulivyokuwa tukicheza,” amesema Jose Mourinho.

Ajax have surprised everyone by progressing through to the Champions League semi-finals

”Unapocheza dhidi ya Ajax, ukacheza kama vile wao wanavyocheza unanafasi kubwa sana ya kupoteza mchezo.”

”Kama kwa mfano Ajax inacheza na Barcelona au Liverpool kwenye hatua ya fainali kama endapo itafanikiwa kuingia, basi nafikiri Barcelona na Liverpool zinauwezo wa kumfunga, hii ni kutokana na uwezo mkubwa waliyokuwa nao timu hizi mbili, lakini kama haupo kwenye ubora kama waliyonao timu hizi basi utalazimika kuwa na mpango wa ziada ili kuifunga Ajax.”

Mourinho believes Tottenham will have to make the game physical to beat Ajax

Ajax imezidi kuwa na nguvu mara baada ya kughairishwa kwa mechi zake zote za ligi inayoshiriki ‘Eredivisie’ mpaka pale itakapo maliza mechi zake Champions League dhidi ya Tottenham mwishoni mwa mwezi huu huko London.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW