AwardsBurudani

Kidedea Cha Kili Awards 2008

Msimu wa Tuzo za Kilimanjaro umemalizika kwa namna yake baada ya wasanii walioshirikia katika kinyang’anyiro hicho baadhi kujinyakulia tuzo zao na wengine kupata nafasi ya kufanya jitihada za kushiriki msimu ujao.

fa_tuzo_1.jpg

 

Msimu wa Tuzo za Kilimanjaro umemalizika kwa namna yake baada ya wasanii walioshirikia katika kinyang’anyiro hicho baadhi kujinyakulia tuzo zao na wengine kupata nafasi ya kufanya jitihada za kushiriki msimu ujao.

Idadi kubwa ya wadau wa masuala ya burudani, wasanii, pamoja na wakuu wa sekta mbali mbali zikiwa ni za serikali na binafsi wote waliweza kuhudhuria katika tafrija hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Kempiski jijini Dar es salaam.

Kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro iliweza kufanikisha azma yake kwa kuwagawia tuzo washiriki ambao wameshinda baada ya kutoa fulsa kwa wananchi kupiga kura kwa njia mbali mbali ikiwa ni kwa njia ya simu na hata mtandao.

Wimbo wa msanii Likiba Cinderella ulimpatia tuzo chipukizi huyo baada ya kushinda katika kipengele kwa Wimbo bora wa R n’B, iliposhindanishwa na nyimbo kama bembeleza ya Marlow, binti kiziwi ya Z-anto, Haiwezekani ya Kasimu na wajua wa Queen Darlin na Alikiba.

Aidha Binti Machozi a.k.a Lady Jay Dee nae hakuwa nyuma katika kinyang’anyiro hicho aliweza kujishindia tuzo ya mwimbaji bora wa kike, baada y kutoka kifua mbele dhidi ya waimbaji wengine wa kike akiwemo Luiza Mbutu, K-lyn pamoja na Sikudhani Ally.

Lakini kwa Bahati mbaya au nzuri Alikiba na Lady Jay Dee hawakuweza kuwepo kuchukua tuzo zao kwani wapo katika ziara nje ye nchi.

Upande wa muziki wa Taarab nao uliweza kumelemeta baada Jahazi Morden Taarab kuibuka kidedea kwa kuwa washindi wa tuzo ya albam bora ya taarab, wakati Dar Morden taarab waliweza kuchukua tuzo ya wimbo bora wa taarab na songi lao Gharika la moyo.

Wimbo wa Asili wa kitanzania tuzo yake ilichukuliwa na Kalunde Band iliyoshinda na kibao chake Itumba mbwene, wakati Albam ya asili ilichukuliwa na Maringo Band kupitia albam yao ya kisiwa cha ukerewe.

Msanii wa Hip Hop Fareed Kubanda a.k.a Fid Q aliweza kucukua tuzo ya wimbo bora wa Hip hop na kibao chake Nia Hayo Tu, Msanii Marlow nae alinyakua tuzo nyingine ya wimbo bora wa mwaka ‘bembeleza’, halikadhalika Khalidi Chokoraa alichukua tuzo ya wimbo bora wa kiswahli ‘kuachwa’ wakati The Africa Stars wana wa Kutwanga na Kupepeta wamechukua tuzo ya Albam bora ‘mtaa wa saba’

Kilimanjaro haikumsahau mkongwe wa dansi Muhidin Gurumo ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Msondo ametunukiwa tuzo ya kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya muziki Tanzania. Gurumo ambaye hakuwepo siku hiyo kwenye tuzo hiz aliweza kupaikana kwa njia ya simu na kusema kuwa “Ninastahili kupata tuzo hiyo, kwani nimetumikia muziki kwa takribani miaka 48 na kufanikiwa kutunga nyimbo zaidi ya 54,” aliyasema alipouwa yuko safarini mkoani arusha na kuongeza kuwa amefarikija kupta kiasi baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.

Wakati tuzo ya Mtunzi Bora wa Muziki ilikwenda kwa Mzee Yusuph, Mtayarishaji Bora wa Nyimbo alikuwa ni Makochali, Mwandikaji Bora wa Nyimbo ni Hamis Mwinyijuma maarufu kama Mwana Fa, Muimbaji chipukizi wa Mwaka ni Maunda Zorro.

Wengine waliotwaa tuzo ni kampuni ya Empty Souls Production (Mtayarishaji Bora wa Video), Bushoke (Wimbo Bora wa Zouk ) na wimbo wa ‘Mbali Nami’ na Ambwene Yessah maarufu Ay na Mwana FA walitwaa tuzo ya Wimbo Bora wa kushirikiana wa ‘Habari ndiyo Hiyo’

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents