Burudani

Kidumu harudi nyuma

Kidumu

Kidumu ambaye jina lake halisi ni Jean Pierre Nimbona anasaka heshima muhimu kwenye Tuzo za Kili Tanzania Music Awards kwa kupitia kibao chake ‘Haturudi Nyuma’ (bofya hapa kusikiliza wimbo huu).

Kidumu, anawania heshima hiyo katika Kipengele Q ambacho ni cha Wimbo Bora wa Afrika Mashariki ambapo anatoleana macho na Blue3, Cindy na Goodlife a.k.a Radio & Weasel.

Katika category hiyo, Kidumu ameingiza nyimbo mbili ambazo ni Haturudi Nyuma ambao amefanya na Juliana Kanyomozi, pia Umenikosea aliougonga mwenyewe.

Nyimbo zote za category hiyo pamoja na namba zake za kuchagua (codes) ni Where you are (12) wa Blue3 ft Goodlife (Radio & Weasel), Haturudi Nyuma (38), Umenikosea (37), Na Wewe (18) wa Cindy na Bread & Butter (68) wa Good Life (Radio & Weasel).

Kupiga kura, unatuma SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi halafu unaambatanisha na herufi ya kipengele (category) kisha namba ya msanii baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723.

Mfano, kuchagua Haturudi Nyuma wa Kidumu na Juliana, unaandika KILI Q38 kisha unatuma SMS yako kwenda namba 15723.

Pia manager wa Kidumu, Sophia Kessy ametoa taarifa kwamba albamu ipo sokoni na inaenda kwa jina la ‘Best of Kidum Haturudi nyuma’.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents